BORA NISINGEOLEWA

  BORA NISINGEOLEWA (Part one)

Mtunzi:Mwl Joshua

0622186752 whatspp/sms/call

``Aweee achana na mimi  eti nisome?, eti nipambane? Kwanini nijisumbue wakati yupo wakunidekeza mie,,,mpenzi wangu ananipenda sana yeye ndio kila kitu kwangu tena nikwambie kitu shoga angu ,nikiolewa mimi nitaishi kama boss we ngoja uone’’ Emmy alijitapa sana kwa wenzake hakuna aliyebishana nae wote walimwitikia tu huku wakimwonea wivu sana kwani Emmy alikuwa na mchumba mwenye fedha nyingi,David mpenzi wa Emmy alikuwa ni kijana mdogo sana mwenye umri wa miaka 26 ,katika umri wake mdogo alibahatika kumiliki hela nyingi na biashara kubwa sana,alifungua maduka makubwa ya nguo mikoani alifungua kampuni mbalimbali, ama kweli kama ni kwa utajiri alikuwa ni tajir wa  nguvu, kwa umri wake mdogo kabisa alikuwa akiitwa boss na wazee kabisa ambao kiumri walikuwa ni sawa au ni zaidi ya baba yake ,kitendo hiki kilimfanya David kuishi kama mfalme alidharau kila mtu aliyekuwa mbele yake kwa jeuri ya hela zake aliamuru kila alichokuwa akikitaka

David alizama katika penzi la emmy wakati Emmy akiwa anasoma chuo cha unesi (nurse) kilichopo Arusha ,kutokana na jeuri ya fedha zake ,David alimtaka mpenzi wake emmy aache chuo haraka

Emmy alisita sana ila baada ya David kurusha shilingi milioni kumi kwa akaunti ya emmy ,emmy alimwamini sana David na moja kwa moja alisitisha masomo na kukaa nyumbani ,familia ya emmy iliishi kwa raha ,mustarehe ,david aliwapa chochote walichokuwa wakikitaka iwe ni fedha au msaada wowote

Siku moja jioni Emmy akiwa kitandani simu ya mpenzi wake David iliita

Huku akitetemeka kwa uoga Emmy aliipokea na kuiweka masikioni

``Hellow sweet’’

``hellow darling pole kwa kazi mpenzi wangu’’

``Asante mpenzi wangu’’

``Niambie Darling’’

``Nimekupigia nakuomba mwisho wa wiki hii tukafungishe ndoa yetu mahakamani nimechoka kuishi maisha haya hela ninayo kila kitu ninacho alfu naishi bila mke mie sasa jiandae alhamisi tunakwenda wajulishe na wazazi wako ‘’

``mhhh dia mbona mapema ‘’

``Unasemaje??’’

Aliuliza david kwa mshangao

Emmy aliogopa kumkwaza mpenzi wake alijibu

``sawa mpenzi wangu haina shida sweet nakaupenda sana na natamani sana tukaishi pamoja nakupenda sana kipenzi cha moyo wangu’’

``ok sawa wajulishe wazee sasa hivi’’

``sawa mpenzi wangu ‘’

Baada ya simu kukatwa kwa haraka emmy alikwenda kuwaeleza wazazi wake juu ya msimamo wa David wa kutaka kufunga ndoa siku ya alhamisi

Kutokana na hofu na mashaka wazazi wa emmy hawakutia neno

Alhamisi ilipofika………………………………………………….

Emy aliolewa rasmi na David walifunga ndoa ya haraka mahakamani ambapo watu wachache walishiriki na baada ya hapo sherehe kubwa ilifanyika nyumbani kwa David ,david hakuweka kiingilio chochote watu walikula kusaza hakika mamilioni ya hela yalitumika kuandaa sherehe ile ,David hakuitisha mchango kutoka kwa mtu yoyote jambo ambalo liliwashangaza watu wengi ila kila mtu alijua hii ni jeuri ya fedha tu

Siku hiyo Emmy alikuwa amepambwa akapambika weupe wake ulimfanya aonekane kama malaika ndani ya shela ,vijana waliokuwa pembeni walikuwa wakimeza mate kwa matamanio kila mmoja alitamani kama emmy angekuwa wake ,vijana waliokuwa wakisoma na emmy chuo kimoja walikuwa wakisema

``Hakika hii ndio nguvu ya fedha ,mzee baba mcheki david anakwenda kulimenya chenza lake nyie mlikuwa mkiliangalia tu kwa macho ‘’

``kwa kweli tulikula kwa macho sasa ndio kaondoka huyo’’

James alidakia maongezi

``Wadau mi nakwambia huyu demu mimi siwezi mwacha hivihivi lazima nipite nae mi nilikuwa namtamani kishenzi’’

``hahahahah we boya kweli mtu ashavishwa pete unasema unapita nae ‘’

``sasa nyie mnabisha kuwadhihirishia hili leo namkiss mbele yenu’’

Kikosi kizima cha vijana kilicheka walimwona James kama mwehu itakuaje mtu amkiss mke wa mtu tena siku ya harusi

``Acha bangi james wewe ‘’

``Ngoja mda wa zawadi uone na mkiss kabisa Yule au nifanye na zaidi ‘’

``ndioooooo’’ wadau waliitikia baada ya kusikia atafanya hivyo muda wa zawadi wakajua lazima atakuwa anamaanisha kabisa

Muda wa zawadi ulipofika ,makundi mbalimbali yalianza kuongozana kutoa zawadi ,matajiri walitoa vitu vya thamani sana mafriji meza za kisasa tv na vitu vingine

James aliona wakati huu ndio wa kujizolea umaarufu alipenyeza na kibahasha chake alichokitia shilingi elfu tano ndani ,alipofika mbele ya bibi harusi alimshika mkono na kumsemesha

``Emyy umenikumbuka my dia ‘’

Emmy alimtazama na kusema

``Si tulikuwa chuo kimoja jina limenitoka ‘’

David bwana harusi alishikwa na hasira sana alikuwa na wivu sana na mke wake kitendo cha james kumshika mkono na kuuminyaminya huku akizungumza nae kilimpandisha hasira mno

Wanachuo walipoona james akiongea na emmy walisogea karibu kusikiliza wengine walipiga picha

James alimsogelea zaidi emmy kitendo kilichomfanya david kubadilika hadi sura emmy hakuwa na cha kufanya kwani alitulia maana watu wengi walikuwa wakimwangalia na akifanya fujo itakuwa kioja

James alimvuta emmy kwa karibu emmy alijitahidi kumsukuma huku akisema

``unataka nini wewe mbona sikuelewi duuh’’

James alimvuta kisha akamkiss kwa nguvu

Picha zilipigwa chapuchapu ,watu walitaharuki sana vjjana wachuo walipiga kelele

``woyooooooo kitu yake hiyooooo ‘’

Machozi yalimtoka emmy kwani alisomeka vibaya hakuna aliyeamini emmy hakuwa na mahusiano na james

David bwana harusi aliposhuhudia emmy akipigwa busu mbele yake alimvuta james kwa hasira na kumkaba watu waliingilia kati kwa haraka na kumwondoa james

Hali ya harusi ilivurugika Mc /mtangazaji alijitahidi kupooza na kusema

``jamani vijana wa sasa huyu kijana kachanganyikiwa na urembo wa bibi harusi anaanza kumbusu halooo ni marufuku jamani kama unatoa zawadi kaa umbali wa mita moja sawa eee’’

Watu walicheka hadi david hasira zilimtoka kidogo na kuanza kucheka ,kweli Mc alitumia hekima sana kupooza

Ila david hakuridhika alichomoa simu na kuandika meseji kwa walinzi wa biashara zake aliwaambia

``Hakikisheni huyu kijana hatoki hapa naomba muondoe uhai wake mara moja hawezi kunivunjia heshima hivi’’

``sawa boss hakuna neno’’

Harusi iliisha watu walitawanyika,vijana walianza kumpongeza james  kwa kumwambia

``mzeee wewe ni hatari sana yaan ume mbusu mtoto mkali kweli huyu lazima utoke nae ‘’

``Yaan huyu kesho mi namtokea ananielewa sana ‘’

Wakiwa wanaondoka

Ghafla james alizungukwa na kikosi cha njemba watatu mmoja akiwa ameshika bastola ,vijana wengine walitamani kupiga kelele ila waliamrishwa

``Kufumba na kufumbua kila mmoja aondoke kabla hatujawalaza shaba’’

James alishikwa na njemba wale kisha alitupwa ndani ya gari ,gari liliwasha mwendo kuelekea asikokujua

Upande wa pili emmy alichukuana na mumewe hadi chumbani kwake ,kilichomshangaza emmy bwana ake alikuwa hana raha hata kidogo ,emmy alimsemesha

``Honey nini shida kipenzi?’’

Kwa hasira david alimkazia macho emmy na kusema

``Emmy unajua ni jinsi gani nilivyokupambani hadi tunafika hapa wewe wakuniaibisha mbele ya ndugu zangu??’’

``Jamani honey mimi Yule kaka sina mahusiano nae aliamua kunichafua tu’’

David alirusha kofi la nguvu na kumpiga emmy

``Paaaaaah ‘’

Emmy alimkazia macho david machozi yalimwagika kama mvua

hakuamini kama mume wake anaweza kumpiga kofi tena siku ya kwanza ya ndoa yao

Je nini kitaendelea

Mpendwa mfuatiliaji soma simulizi hii mwanzo mwisho kwa elfu moja tu unapitwaje na uhondo cha kufanya lipia elfu moja sasa kwa namba 0742873299 martha shayo baada ya hapo njoo whatsapp au facebook inbox nikupe yote whatsapp 0622186752

Usipitwe na uhondo huu fanya malipo sasa 


No comments

Powered by Blogger.