Hugo Kocha Mpya Afrika kusini

 

MICHEZO

Hugo kocha mpya Afrika kusini.

Shirikisho la soka Afrika Kusini (SAFA) limemtangaza Kocha Hugo Henri Broos (69) raia wa Ubelgiji kuwa Kocha wao mpya.

Hugo amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuifundisha Afrika Kusini na anatajwa kuwa atakuwa akilipwa mshahara wa USD 50,000 (Tsh milioni 115.9) kwa mwezi.

Kocha Hugo aliwahi kuwa Kocha wa vilabu kadhaa Ulaya kama Club Brugge, KRC Genk na timu ya Taifa ya Cameroon, mara ya mwisho 2019 alikuwa Kocha wa muda wa KV Oostende.

No comments

Powered by Blogger.