Onyo la Korea kaskazini kwa marekani Duh hatari.


 Korea Kaskazini imepuuza wazo la kufanya mazungumzo na Marekani siku moja baada ya Utawala wa Marekani kusema uko tayari kwa majadiliano ya kidiplomasia kuhusu Korea Kaskazini kuachana na mradi wake wa nyuklia.

Korea Kaskazini imesema haiko tayari kufanya mazungumzo na Marekani wakiliita Taifa linalotumia diplomasia bandia kuficha matendo yake ya uchokozi.

Taifa hilo pia limemtahadharisha Rais Joe Biden wa Marekani dhidi ya kuchukua waliouita msimamo uliopitwa na wakati na kuonya kuwa Marekani itapata madhara kwa kuichokoza Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini inatoa kauli hiyo siku kadhaa tangu Rais Biden alipoliambia Bunge la Marekani kuwa Utawala wake utatumia diplomasia pamoja na msimamo usioyumba kudhibiti malengo ya nyuklia ya Korea Kaskazini

#Korea#Biden#mh

By swidhan mapunda

No comments

Powered by Blogger.